Lyric Video Imekuwa ni Fashion Kwa Wasanii Bongo, Wasanii Wakubwa Nje Hawafanyi


Nimejaribu kupitia kwenye channels kadhaa za wasanii wa nje ni nadra sana kukutana na lyric videos zimekuwa uploaded kwenye channels zao, ila hii bongo ilianza kimasihara na sasa imekuwa donda ndugu, kila msanii anataka aweke kwanza lyric video kabla ya kuachia official music video.


Simaanishi tuwaige wao kutofanya, ila hivi vitu vifanyike pale panapo hitajika, either msanii hana mpango wa kuachia video rasmi ya wimbo husika, ama kuimba lugha ambayo haishabiiani na jamii mama na kingine Lyric video background yake inapaswa kuwa plane kama dhamira ya msanii ni watu wasome lyrics zake, vinginevyo ni ujanja ujanja tu. Ni ngumu sana hii leo nirudie kuangalia Mahaba ya Alikiba wakati nishaona namna alivyo podoka kwenye lyric video.


Sidhani kama ni njia sahihi pia ya kukuza kipato maana wengine wamefosi hadi kushuti kwenye Matikiti, wanaorudia kutazama official music video ni wachache sana baada ya kutazama Lyric video, hivyo idadi ya walioview Aina hizo za video, ni hao hao ambao wangeview official video. Tufanye lyric video ina 400k views, official ina 1M views, ni rahisi official video kuwa na 1.4m pia.


Bongo kitu kikianza hadi kero kama listening parties za projects za wasanii wetu, kila mmoja atataka kufanya, na hii inafanya ziwe za kawaida sana, hakuna ubunifu wowote zaidi ya ___ INVITED, Tangu Kanye West amesumbua na Listening party zake za Donda 2021 ni kama aliwashtua wana huku bongo waanze fujo za Listening Parties.


Wasanii Badilikeni! kuna vitu vingi mnaweza buni na mka-upload kwa YouTube channels zenu kama ishu ni kukuza chambi chambi.

By Soja Media

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad