Madaktari wa Yanga Waokoa Maisha ya Abiria Ndani ya Ndege




Ilikuwa hivi…….

Wakati ndege ikiwa angani saa mbili kabla ya kutua nchini Tunisia, rubani alitangaza kuomba msaada akisema, “….tunaomba kama kuna daktari yeyote ndani ya ndege hii apite mbele, tuna mgonjwa yupo katika hali ya hatari”.

Punde jopo la madaktari wa Yanga lilipita mbele na kwenda moja kwa moja kumsaidia abiria mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja.

Kwa mujibu wa maelezo ya daktari wa Yanga, Moses Etutu, abiria huyo pamoja na matatizo mengine ya kiafya, alikuwa na changamoto ya sukari. Walimpa huduma ya kwanza na hatimaye hali ya abiria ikaimarika.

Kwa mujibu wa taarifa ya wahudumu, ndege hiyo ya Shirika la Ndege la Emirates ilipanga kutua katika Uwanja wa Ndege wa karibu ili kuokoa maisha ya abiria huyo lakini kutokana na jitihada za madaktari wa Yanga, safari iliendelea hadi kutua Jijini Tunis kwa wakati.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad