Maelfu wajitokeza kuasili kichanga kilicho okolewa kwenye kifusi

 


Maelfu ya watu wamejitokeza kutaka kumuasili mtoto wa kike aliyezaliwa chini ya vifusi vya jengo lililoporomoka kaskazini-magharibi mwa Syria, kufuatia tetemeko la ardhi la Jumatatu.


Mara baada ya kuokolewa, mtoto huyo aliyepewa jina la Aya jina lenye maana ya neno muujiza (kwa Kiarabu), ambaye bado kitovu chake kilikuwa kimeungana na mamake aliyejifungua kwenye kifusi ambapo mama na baba wa mtoto huyo, na ndugu zake wote wanne walifariki baada ya tetemeko hilo kupiga mji wa Jindayris.


Daktari wa watoto anayemuhudumia mtoto huyo, Hani Marouf amesema, “alifika Jumatatu akiwa katika hali mbaya sana, alikuwa na michubuko, alishikwa na baridi na alikuwa anapumua kwa shida.” na kwasasa Kwa sasa, mkewe na Dkt. Attiah ndiye anayemnyonyesha.


Video za uokoaji wa mtoto Aya, zilienea kwenye mitandao ya kijamii. Picha zilionyesha mwanamume mmoja akikimbia kutoka kwa kifusi cha jengo lililoporomoka, akiwa amemshikilia mtoto mchanga aliyekuwa ameenea vumbi.


Maelfu ya watu kwenye mitandao ya kijamii sasa wamekuwa wakiomba maelezo ya namna ya kumuasili ambapo Mtangazaji wa televisheni ya Kuwait alisema, “Niko tayari kumtunza na kumlea mtoto huyu… ikiwa taratibu za kisheria zitaniruhusu.”


Meneja wa hospitali anakohudumiwa mtoto huyo, Khalid Attiah, anasema amepokea simu nyingi kutoka kwa watu kote ulimwenguni wakitaka kumuasili mtoto Aya huku Dkt. Attiah anayemuhudumia na ambaye ana binti mchanga wa tofauti ya minne akisema, “Sitaruhusu mtu yeyote kumlea kwa sasa hadi itakapopatikana familia yake, ninamchukulia kama mmoja wa watoto wangu.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad