Man City Hatihati Kushushwa Daraja Kutoka Ligi Kuu Ya England Au Kukatwa Pointi



MANCHESTER City huenda ikakabiliwa na adhabu ya kushushwa daraja kutoka Ligi Kuu ya England au kukatwa pointi kwa kosa la kuvunja sheria za fedha zaidi ya mara 100 kuhusu mikataba ya udhamini, mikataba ya siri na malipo.

Manchester City wameshtakiwa na Premier League kwa kukiuka sheria hizo. Mashtaka dhidi ya mabingwa hao watetezi yanahusiana na taarifa za fedha kuhusu mapato, maelezo ya malipo ya makocha na wachezaji, kanuni za UEFA, faida na uendelevu na ushirikiano na uchunguzi wa Ligi Kuu.

Taarifa kutoka kwenye ligi hiyo ilisema ukiukaji huo unaodaiwa ulifanyika kuanzia Septemba 2009 hadi msimu wa 2017-18 na sasa utatumwa kwa tume huru ili kuchunguza. City pia wanakabiliwa na mashtaka ya kushindwa kushirikiana na uchunguzi huo ulioanza Desemba 2018.

Inaongeza kuwa klabu hiyo inadaiwa kukiuka kanuni za ligi zinazohitaji kutolewa kwa nia njema kabisa ya taarifa sahihi za kifedha zinazotoa mtazamo wa kweli na wa haki wa hali ya kifedha ya klabu.

Iwapo Man City watapatikana na hatia, watakabiliwa na vikwazo vingi ikiwa ni pamoja na kukatwa pointi au hata kushushwa daraja ingawa mchakato huo unaweza kuchukua miaka kadhaa kufikia tamati.

Klabu bado haijatoa maoni yoyote lakini, Sportsmail inaelewa kuwa wako tayari kujilinda kwa nguvu zote.


Kati ya tarehe zilizotajwa, Man City ilishinda mataji matatu ya Ligi Kuu, Kombe la FA na Vikombe vitatu vya Carabao.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad