Ikiwa ni siku 14 tu tangu kutokea kwa Tetemeko la Ardhi lililoua zaidi ya Watu 47,000, taarifa mpya ni kuwa kumetokea Matetemeko mengine mawili kwenye Miji ya Antakya na Adana na mpakani mwa nchi hizo.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa majengo kadhaa yameharibiwa katika miji hiyo ingawa bado hakuna ripoti haraka za madhara kwa binadamu.
Matetemeko hayo yenye ukubwa wa ritcher 6.4 na 5.8, watalaamu wameeleza kuwa yawezekana tetemeko hili ni sehemu ya tetemeko lililopita hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Mamlaka, ndani ya wiki 2, yamerekodiwa Matetemeko zaidi ya 6,000 baada ya Tetemeko la awali lililosababisha madhara kwenye Nchi za Syria na Uturuki.