Mbunge Afukuzwa Bungeni Kisa Madoa ya Damu ya Hedhi Katika Suti Yake


Seneta wa Kenya alifukuzwa bungeni baada ya kuhudhuria kikao akiwa amevalia suti nyeupe iliyokuwa na alama rangi nyekundu (kuashiria hedhi) katika kampeni inayoonekana kuwa ya harakati za kushinikiza upatikanani wa taulo za hedhi.

Gloria Orwoba, wa muungano unaotawala, anatarajiwa kuwasilisha hoja kuhusu mswada wa kutoa taulo za bure siku ya Jumatano kama sehemu ya juhudi za kumaliza umaskini wa muda.

Maseneta walitatiza kikao cha Jumanne alasiri ili kumfahamisha spika kwamba Bi Owoba alikuwana "mavazi yasiyofaa".

Lakini seneta huyo alipinga akisema: "Nashangaa kwamba mtu anaweza kusimama hapa na kusema kwamba bunge limefedheheshwa kwa sababu mwanamke amepata hedhi."

Spika Amason Kingi aliamuru seneta huyo kwenda kubadilisha nguo zake kabla ya kureruhusiwa tena bungeni.

“Sio kosa kuwa na hedhi... Seneta Gloria nasikitika unapitia hali ya kimaumbili, suti yako imepata madoa ya ajabu, naomba uondoke ili ukabadilishe urudi na. nguo ambazo hazina madoa," msemaji alisema.

Nje ya ukumbi, Seneta Owoba aliwaambia waandishi wa habari:

“Tunalenga kutokomeza janga linalotokana na unyanyapaa wa hedhi. Baadhi ya mambo ambayo ninayotetea na kubuni sheria na kuhakikisha kwamba tunatoa bure taulo za hedhi kwa watoto wote wanaokwenda shule." from Gloria Orwoba

Tunalenga kutokomeza janga linalotokana na unyanyapaa wa hedhi. Baadhi ya mambo ambayo ninayotetea na kubuni sheria na kuhakikisha kwamba tunatoa bure taulo za hedhi kwa watoto wote wanaokwenda shule."
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad