Mkoa wa Morogoro Ndio Tunu ya Sanaa Tanzania, Umetoa Vipaji Vingi



Mkoa wa morogoro ndio tunu ya sanaa, burudani na michezo Tanzania. Huo mkoa umetoa vipaji adhimu na adimu sana na ndio tegemeo kubwa kwa taifa kwenye kuzalisha burudani na michezo.

Huwezi kuulinganisha mkoa wa morogoro kwenye burudani na michezo na mkoa wowote ule hata kigoma licha ya Kutoa Mastaa baadhi bado ipo mbali na itasubiri kwa morogoro

KISOKA
Ukiachana na timu za Dar Morogoro inafuatia kuwa na timu nyingu zilizowahi kutwaa taji la ligi kuu nazo ni Mtibwa Sugar na Mseto ukiachana na Tukuyu stars ya Mbeya hakuna mkoa uliowah kufanya hivyo hapa Tz..na kuna timu ilikuwa inaitwa reli "kiboko ya vigogo" Simba na Yanga zilikuwa hazitoki zikicheza na timu hii

Morogoro ni nyumba ya vipaji vya soka tangu zamani Kina Mohamed Msomali, Malota Soma, Zamoyoni Mogella, Charles Boniface Mkwasa(aliyelelewa na Dada yake mtaa wa karume Morogoro tangu akiwa kijana mdogo) na wengineo magwiji wa zamani,kwa sasa wapo kina Mkude kibabage,Dickson Job,Aishi Manula,Kelvin wa Genk,Shomari Kapombe,Kibwana Shomari n.k

NGUMI
Hakuna asiyejua kwamba ukitoa Dar Moro ina ufalme wake katika ngumi Francis Cheka,Cosmas Cheka,Twaha Kiduku,Mandonga Mtu Kazi na wengine kibao wanatoka Morogoro

MUZIKI
Zamani watu Dansi walikuwa wanalifuata Moro kutoka Dar kuwaona Cuban Marimba ya Salum abdallah na baadae Juma Kilaza na Moro Jazz Band ya Mbaraka Mimi Mwishehe. Moro Jazz Band ni ya miaka 1930's

Wasanii wa Morogoro kwa sasa ni Rich Mavoko, Jay Melody, Belle 9, Dayna, Conboi, Tundaman na wengineo hata Sallam, Babu Tale wanatokea Morogoro

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad