Mo Dewji Atangazwa Kuwa Bilionea Wa 13 Afrika, Apanda Kwa Nafasi Mbili



Bilionea na mfanyabiashara maarufu Tanzania na Afrika kwa ujumla, Mohammed Dewji, anazidi kupaa kwa utajiri duniani baada ya hivi karibuni Jarida la Fobes kutoa orodha ya mabilionea 19 Afrika.


Katika orodha hiyo iliyotoka Januari 30, 2023, Mo Dewji ambaye ni Rais wa Heshima wa Klabu ya Simba, ameshika nafasi ya 13 kutoka 15 aliyokuwa awali, akiwa na utajiri wa Dola za Marekani bilioni 1.5.


Mo Dewji ambaye ameongeza ajira hadi 35,000 kutoka 28,000, ndani ya Afrika Mashariki yupo pekee yake kwenye orodha hiyo ya Jarida la Fobes, hiyo inadhihirisha wazi kwamba, kwa ukanda huu, yeye ndiye bilionea namba moja.


Kwa mujibu wa Fobes, orodha hiyo imezingatia utajiri wa mabilionea wa Kiafrika ambao wanaishi Afrika au wana biashara zao barani humo.


Mo Dewji ambaye ni mwanamichezo, katika orodha ya Fobes, inaonesha utajiri wake unatokana na vyanzo mbalimbali vya mapato huku akiwa na viwanda vingi vilivyotoa ajira kwa kundi kubwa la raia wa Tanzania.


Mnigeria Aliko Dangote ameendelea kuwa namba moja akiwa na utajiri wa Dola za Marekani Bilioni 13.5.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad