Mrembo Amber Rose Anyoosha Maelezo "Nilimpenda zaidi Wiz Khalifah Kuliko Kanye West Aliyenipa Umaarufu"

Mrembo Amber Rose Anyoosha Maelezo "Nilimpenda zaidi Wiz Khalifah Kuliko Kanye West Aliyenipa Umaarufu"

Wakati ulimwengu unaanza kujua #amberrose ni nani, alikuwa yupo mikononi mwa #kanyewest kama Boyfriend wake, kiufupi Kanye West ndiye aliye mtambulisha zaidi Amber Rose kwenye ulimwengu wa umaarufu, licha ya yote hayo, Amber Rose ameketi kwenye podcast interview inayoitwa GUYS WE FED iliyoruka hewani January 21, 2023, ambapo miongoni mwa maswali aliyoulizwa, ni Ex yupi kati ya Kanye West na Wiz Khalifah alimpenda zaidi wakati akiwa nao kwenye mahusiano.


Rose kanyoosha mstari kuwa, Wiz Khalifah ndiye mwanaume pekee ambaye amewahi kumpenda tangu aanze kuwa kwenye mahusiano na wanaume tofauti na sio Kanye West ambaye kiukweli hakumpenda japo alimpa nafasi ya kufahamika. Rose amedai bado anampenda Wiz na si kumpenda tu bali wanapendana hadi sasa, namna wanavyo ongea namna wanavyo jaliana, unayaona mapenzi ya dhati kati yao ukiachilia mbali wao kuwa na mtoto pamoja na pia kutokuwa pamoja kwa sasa.


Hivi karibuni Amber Rose alitweet kuwa Ye ni mtu anaye penda zaidi ngono licha ya Ye kukataa madai hayo. Wataalamu wa mambo wanadai kinacho msukuma Amber Rose kudai hampendi Kanye, ni kwadababu ya Kanye West kumtukana Wiz Khalifah na kudai bila Yeye hasingekuwa na mtoto na Amber Rose, akidai pia anammiliki mtoto wake. Hili pia lilikuja baada ya Wiz Khalifah kudiss album ya Kanye West inayoitwa Waves na West akihisi miongoni mwa tweets za Wiz zilimlenga hadi Kim Kardashian.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad