Mtuhumiwa Korogwe Hakujinyonga Ndani ya Mahabusu - RC Mgumba

 


Mkuu wa mkoa wa Tanga Omary Mgumba amesema mahabusu anaedaiwa kufia kwenye chumba cha mahabusu amefia uraiani na kwani tayari watuhumiwa hao walikuwa wamefikishwa mahakamani na kupatiwa dhamana 



Mgumba amesema hayo wakati akizungumza kwa njia ya simu katika kipindi cha Supa Breakfast kinachoruka East Africa Radio Jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa 11 Alfajiri hadi saa 3 Asubuhi ambapo amesema 


“Waliokuwa mahabusu sio mahabusu kwa sasa,tuliwafikisha  mahakamani na  walipata dhamana na walikuwa nje  na  hata hili tukio la kujinyonga halijatokea mahabusu  bali  limetokea uraiani “


Mgumba ameongeza kuwa Siku ya kuripoti mahakamni ambayo ilikuwa tarehe 22 February mwaka huu Bw.Said Charles ambaye ndie mahabusu anaedaiwa kujinyonga hakutokea mahakamani siku hiyo na mototo wake ambaye alimuwekea dhamana kurudi uraiani  baada ya kutomuona kutomuona katika viunga vya mahakama  alipata wasiwasi na kuanza kumtafuta 


Ameongeza kuwa sikuya jana wajukuu zake ndugu na jamaa walifanikiwa kumuona katika shamba lake akiwa amejinyonga kwenye mti


“Wajukuu zake,ndugu na marafiki walifanikiwa kumuona huko shambani kwake akiwa amejinyonga kwenye mti kwa kutumia Neti ya Mbu na baada ya hapo walitoa taarifa polisi na timu ya uchunguzi ndio ikaenda eneo la tukio “ Alisema Mgumba “


Amemaliza kwa kusema kuwa Taarifa za kuwa alijinyonga akiwa ndani ya chumba cha mahabusu zipuuzwe na sio sahihi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad