Mudathir Yahya Atengenezewa Kombinesheni Mpya Yanga


 

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nasreddine Nabi amevutiwa na muunganiko mpya wa safu ya kiungo ya timu hiyo, iliyocheza mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.


Mtunisia huyo kwa mara ya kwanza alitumia viungo watatu wakabaji katika mchezo dhidi ya TP Mazembe uliochezwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar na Yanga kushinda kwa mabao 3-1.


Katika mchezo huo, Nabi aliingia na sapraizi akiwaanzisha viungo ambapo ni Khalid Aucho aliyecheza namba 8, Yannick Bangala (6) na Mudathiri (10).


Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, kocha huyo amepanga kuiboresha safu hiyo zaidi kwa kuwaongezea mbinu za kiufundi zitakazowafanya wacheze kwa kuelewana.


Mtoa taarifa huyo alisema mfumo huo atautimia kutokana na aina ya timu atakayokutana nayo ambayo inaanzisha mashambulizi golini kwao kwa lengo la kuwazuia kufika mbele.


Aliongeza kuwa, upo uwezekano mkubwa wa kocha huyo, kumrejesha Bangala katika nafasi hiyo ya kiungo namba 6 kutoka beki wa kati namba 5 baada ya kuvutiwa na aina yake ya uchezaji ya kupunguza mashambulizi golini kwao.


“Kocha Nabi amevutiwa na jinsi viungo wake Bangala, Aucho na Mudathiri walivyotimiza majukumu yao vizuri sambamba na kuelewana kwa muda mfupi wakicheza pamoja katika mchezo dhidi ya Mazembe.


“Ilikuwa sapraizi kubwa kwa mashabiki wa Yanga, pia wapinzani wetu kwa kumuanzisha Mudathiri kucheza namba 10 badala ya 6 na 8 ambazo amekuwa akicheza michezo iliyopita.


“Pia Bangala kumrejesha katika nafasi yake ya kiungo namba 6, mashabiki walifurahia kumuona mchezaji huyo akicheza nafasi hiyo ambayo kila Mwanayanga anapenda achezeshwe hapo.


“Katika mchezo dhidi ya Mazembe, Nabi amefurahia jinsi walivyocheza viungo hao na kuifanya timu kuwa imara na kumiliki safu ya kiungo, hivyo amepanga kuwaongezea mazoezi ya kimbinu na kiufundi zaidi ili wawe na muunganiko mzuri,” alisema mtoa taarifa.


Akizungumzia hilo, Nabi alisema kuwa: “Nitaendelea kuwatumia viungo hao kucheza pamoja katika baadhi ya michezo ambayo wapinzani wetu ni wazuri kuanzia chini katika kuanzisha mashambulizi.


“Sababu ya kumuanzisha Mudathiri kucheza namba 10, ni suala la kimbinu zaidi ni baada ya kuwaona kuiona michezo yao ya mwisho ya kimataifa na ligi ambayo wameicheza, hivyo nikaingia kwa mbinu ya kuwazuia kuanzia juu.”


STORI: WILBERT MOLANDI

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad