Mwanafamilia na Shuhuda wa ajali iliyoua Watu 17 Asimulia A to Z, Aomba Msaada wa Kuzika


Mwanafamilia na Shuhuda wa
ajali iliyoua Watu 17 Mkoani Tanga, Ginesi Mrema ameiomba Serikali na Wadau wengine kuwasaida kufanikisha mazishi ya Wapendwa wao ambapo amesema Watu 14 waliofariki ambao walikuwa kwenye Coaster iliyobeba maiti wote ni Ndugu wa Ukoo mmoja wa Mrema na ajali ilipotokea wameibiwa vitu na fedha hivyo hawana tena fedha za kugharamia mazishi.

Ajali hiyo imetokea usiku wa jana Wilayani Korogwe na kusababisha vifo 17 na majeruhi 12 na imehusisha kugongana kwa gari ya fuso na gari ya abiria(Coaster) ambayo ilikuwa imebeba maiti iliyokuwa inatokea Dar es salaam kwenda Mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.

“Aliyefariki ni Baba Mdogo alikuwa anaishi Mbezi kwa Msuguli akaanza kuumwa tukampeleka Hospitali akafariki, jana tukachukua mwili tukawa tunaenda Mkuu Rombo kuzika, tumefika Korogwe ile gari iliyokuwa na Wanafamilia ikagonganga uso kwa uso na fuso wakafariki Ndugu zetu 14 na kwenye fuso walikuwepo watatu idadi ikawa 17”

“Watoto wa Marehemu waliofariki ni Mwanae mkubwa Nesto na Mdogo wake anayemfuata anaitwa Augustina wote wawili wamefariki, kwa upande Baba yangu ambaye sisi tunamuita yule Baba mdogo wamefariki wawili na Dada yangu alikuwa na yeye na Mwanae kafariki palepale, na hao wengine waliofariki kuna Watoto wa Baba mkubwa yaani Majirani ambao wamezunguka palepale”

“Dereva ambaye alikuwa na hii gari ya msiba alikuwa anaover-take pembeni yake upande wa kushoto kulikuwa na fuso, yule alipooona vile akailaza pembeni ikaja fuso inayokuja kwa mbele zikagongana uso kwa uso na gari ya msiba”

“Msiba ni wa ukoo wa Mrema na wote 14 waliofariki ukiacha wa fuso ni ukoo mmoja na wote ni Majirani kwasababu ni Ndugu wa Familia moja ambao tuko sehemu moja wote, nawapa taarifa Ndugu, Jamaa na Marafiki wa Ukoo wa Mrema tushirikiane, Serikali pia kwasababu suala limekuwa kubwa sana Wanafamilia msiba ulipotokea wameibiwa vitu vyao, hata Mtoto wa Marehemu ambaye alikuwa na pesa wameiba palepale kwahiyo sisi tunahitaji msaada ili tufanikishe hili suala”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad