Taasisi ya tiba ya mifupa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI) imesema Mwanaume aliyeonekana akigongwa na Basi la abiria “mwendokasi” Jijini Dar es salaam jana, amelazwa Hospitalini hapo kwenye chumba cha Uangalizi Maalum (ICU).
Meneja wa Kitengo cha Uhusiano cha MOI Patrick Mvungi ameiambia @AyoTV_ kuwa Mtu huyo wamempa jina la ‘UNKNOWN’ kwa sababu mpaka sasa hawana taarifa zake rasmi.
Mvungi ameongeza kuwa mpaka sasa Mtu huyo ambaye amevunjika mguu, mkono na kuumia kichwani hawezi kuongea lakini anafungua macho