Mwimbaji Nyota wa RnB, Chris Brown Awatolea Uvivu Wanaoendelea Kumuhukumu Tukio la Kumpiga Rihanna


Mwimbaji nyota wa RnB, Chris Brown ameamua kuwatolea uvivu wale wote ambao wanaendelea kumhukumu na pia kumkandamiza kwa tukio la kuwahi kumpiga Rihanna, mwaka 2009 wakati huo wapo kwenye mahusiano na akiwa na miaka 17.


Breezy ambaye ameonesha kuwa mwenye hasira katika ujumbe wake kupitia insta story yake ameeleza kwamba ana miaka 33 sasa, na tukio hilo alilolifanya lina miaka 14, hivyo amechoshwa na nyote mnaoendelea na huo mjadala akiwatolea mfano Blueface na Chrisean wakipigana Dunia nzima inawatazama je hivyo ni sawa! Amehoji.


"Kama nyie wote bado mnanichukia kwa kosa nililofanya nikiwa na umri wa miaka 17, tafadhali, Nina miaka 33 sasa, nimechoshwa na nyote mnaoendelea kuzunguka na huu mjadala.


Nyie ndio wale wale ambao huwa mnatulia kila wiki kuangalia Blueface na Chrisean wakipigana mbele ya dunia nzima. Lakini hilo ni sawa? Ni la kuburudisha?" Alimaliza Breezy kwenye ujumbe wake.


"Ziko wapi hizi tamaduni za kushauri wasanii weupe wanaotoka kimapenzi na wasichana wenye umri mdogo, wanaowapiga wake zao na kuwapa virusi vya Ukimwi?.... Oooh hiyo imekaa sawa eeh, ni washkaji zenu. Hakuna tena upendo wa kinafki kutoka kwangu, kaeni mbali na mimi. Hakuna kati yenu na mimi anayeweza kunizingua" - ameendelea kueleza kwenye ujumbe wake mwingine.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad