Said Kibula (69) aliyekuwa akituhumiwa kwa uporaji wa mali za watu waliokufa katika ajali ya Coster iliyokuwa ikisafirishwa maiti kupelekwa Rombo kwa mazishi amezikwa leo Februari 24, 2023 kijijini kwake Magira Gereza wilayani Korogwe.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, David Chidinga, mtuhumiwa huyo alijinyonga usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita shambani kwake kwa kutumia chandarua.
Imeelezwa kuwa, Kibula ambaye awali alishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na uporaji wa mali za waliokufa katika ajali hiyo, baada ya kukamilika kwa upelelezi alifikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Mombo na baadaye alipewa dhamana na kurejea nyumbani kwake.
Alisema Ali Said ambaye ni mtoto wa marehemu amesema marehemu alienda shuleni kwa mjukuu wake na kumpa Sh2,000 na manati baadaye hakuonekana tena hadi siku ya pili saa 2 asubuhi alipokutwa amejinyonga kwenye mti wa mwembe.
Wakati kaimu kamanda akitoa maelezo hayo, mkuu wa mkoa wa Tanga, Omary Mgumba jana akizungumza suala hilo katika kikao cha utiaji saini mikataba ya miradi ya maji akisema amefia kituo cha polisi