Zaidi ya watu 1,200 wanadaiwa kufariki baada ya tetemeko la ardhi la Ardhi kutikisa kusini mashariki mwa Uturuki na kaskazini mwa Syria mapema Jumatatu.
.
Maafisa walisema Tetemeko hilo limetokea katika mji wa Pazarcik katika mkoa wa Kahramanmaras kusini-mashariki mwa Uturuki na kufuatiwa na matetemeko kadhaa yenye nguvu. Maelfu ya majengo yamebomolewa pande zote mbili za mpaka, na idadi ya vifo ilitarajiwa kuongezeka huku waokoaji wakitafuta manusura kwenye mirundiko mikubwa ya vifusi. Uturuki na Syria zimetangaza hali ya hatari.
.