Polisi yafukua kaburi kumaliza utata kijana aliyeonekana mtaani



Kigoma. Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi na wataalamu wa afya, wamefukua kaburi la kijana Henry James (28), aliyedaiwa kufariki Aprili 20, 2022 na kupatikana akiwa hai Desemba 22,2022.

Tukio hilo la ufukuaji wa kaburi umefanyika katika Kijiji cha Kandaga, wilayani Uvinza leo Januari 22, 2023 na kukutwa mwili huo ambapo wamechukua sampuli na kupelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali kwa ajili ya uchunguzi wa vina saba.

Lengo la ufukuaji huo wa kaburi linalodaiwa la kijana Henry ni kupata sampuli za vinasaba vya mwili huo na kulinganisha na sampuni za kijana huyo huyo anayedaiwa kuonekana uraiani akiwa hai mwishoni mwa mwaka jana.

Ikumbukwe Aprili 19,2022 katika eneo la Mazungwe Wilaya ya Uvinza, ilitokea ajali ya gari kugonga mtu na kufariki, ambapo ndugu wa kijana huyo walifika katika kituo cha afya Kazuramimba na kudai aliyefariki kwenye ajali hiyo ni ndugu yao na kufanya taratibu zote za mazishi baada ya kukabidhiwa mwili na Jeshi la Polisi.


Januari 2, 2023 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Filemon Makungu alitoa taarifa ya kukutwa hai kwa kijana huyo ambaye alibainika kuwa na tatizo la afya ya akili na kwamba atafanyiwa uchunguzi wa kisayansi ili kujua ukweli wa yule aliyefariki na aliyekutwa akiwa hai.

Kamanda Makungu alisema pamoja na mama mzazi wa kijana huyo, Schola Bukuku  kukiri kumtambua mtoto wake na kudai awali alishiriki mazishi ya mwanaye lakini kitendo cha kuonekana tena ni majibu ya maombi yake aliyokuwa akiomba kwa Mungu baada ya kifo cha mwanaye.

“Tunawaomba wananchi watulie wakati jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa kifo cha kijana huyo kuonekana uraiani akiwa hai, yani tunafanya uchunguzi wa kisayansi ili kujua ukweli wa yule aliyefariki na huyu aliyeokotwa akiwa hao,” amesema kamanda Makungu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad