Rais Apiga Marufuku Wanawake Kutumia Jina Linalofanana na la Binti yake

 


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un ametoa katazo kwa familia na watu wengine wa Taifa lake kwamba hakuna ambaye anaruhusiwa kuwa na Jina kama la binti yake Ju Ae (Kim Ju-Ae) mwenye umri wa miaka 10.


Kiongozi huyo amekuwa akionekana mara nyingi akiwa na binti yake huyo kwenye maeneo mbali mbali kiasi cha kutengeneza maneno anaweza kuwa mrithi wake.


Kim Jong-Un ametoa amri hiyo kwamba yeyote ambaye ana jina kama la binti yake anatakiwa kubadilisha hadi wiki ijayo.


Kwa mujibu wa Radio Free Asia, mwanamke mmoja ambaye naye anaitwa Ju Ae, alitumiwa ombi la kubadili jina hilo mara moja.


Hii sio mara ya kwanza kwa agizo kama hilo kutoka kwa watawala wa Korea Kaskazini, Kiongozi wa zamani wa taifa hilo Kim II-Sung alipiga marufuku kama hiyo kwa mtu yeyote kutumia jina kama lake kipindi anaingia madarakani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad