Siku ya Jana Feb 04 kumefanyika fainali za #bongostarsearch ikiwa ni msimu wake wa 13 tangu kuanzishwa kwake ambapo mshindi wa shindano hilo ni Asagwile Mwasongwe ambaye ameshinda kiasi cha milioni 20 Tsh, mshindi wa pili akiwa ni Leonard Sanga aliyeondoka na Sh. Milioni 3 Tsh na mshindi wa tatu ni Patrick Alsina aliyeokota milioni 1.
Tunajua lengo la @bongostarsearch ni zuri, kusaidia kuibua vipaji vilivyo mtaani ambavyo kwa namna moja ama nyingine vimeshindwa kuonekana, Lakini haishii hapo bali kuwapa chochote kitu kama zawadi ya wao kufika kwenye nafasi za juu zaidi.
Ebu mfikirieni mshindi wa 2 na 3 vizur, ebu vaeni nafsi zao muhisi namna wanavyo jisikia, tuache kujificha kwenye kichaka cha “suala sio pesa kikubwa mtu kapata platform ya kuonekana”, mi Naamini hata aliyeshika nafasi ya 20, ameonekana kwenye platform hiyo hiyo moja, ila je, hiyo platform inatengeneza ushawishi upi kwa watu kuona hivi sasa?
Imagine kwa safari yote hiyo ndefu mshindi wa wa pili anapata milioni 3, mshindi wa tatu milioni 1, like serious?, si bora iwe wazi kuwa pesa atapewa mshindi pekee! Ni kweli mmejitoa kusaidia, basi saidieni kikamilifu, kama serikali inaweza mkopesha mwanamuziki milioni 40, sifikirii kama mkikaa nao meza moja mkaongea vizuri, itashindwa kudonate kiasi fulani cha zawadi ya washindi wa Fainali hizi. Angalau ingekuwa 20, 10 kwa mshindi wa pili, 7/5 na mshindi wa 3.
Mfano Britain Got Talent au America Got Talent, Wanaoshika nafasi ya pili na kuendelea hawapati zawadi ya pesa kama anavyopata mshindi wa kwanza, ila wanakuwa tayari wamepata endorsements kiasi kwamba wanaanza ingiza pesa punde tu baada ya kumalizika kwa mashindano hayo, kwakuwa hata mazingira ya mashindano yao ni yenye ushawishi, hufuatiliwa na wengi.
Jana ilikuwa ni fainali, ila wengi hawajui kama ilikuwa fainali, hii ni Ishara kuwa BSS inapoteza mvuto, tunawasaidiaje hawa wanaopata milioni 1 kama zawadi kuonekana kwa watu wenye bidhaa zao? Ileteni BSS kwenye Channel za Bure watu wafuatilie kwa wingi ili kuwajenga contestants, kama shida ni mdhamini, ongeeni na serikali kuhusu hili, kwa hapa, Startimes wananufaika zaidi kuliko shindano lenyewe linavyo nufaika.
Naongea na BSS.
Ameandika : Sajomedia