Sakata Mkataba Fei Toto, Yanga





KUTOKANA na mvutano mkubwa uliopo kati ya uongozi wa klabu ya Yanga na kiungo wa timu hiyo, Feisal Salimu ‘Feitoto’, ambao bado haujapatiwa suluhisho, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini, Ally Mayay, ameibuka na kuwataka kutumia busara kuweza kulimaliza suala hilo.

Mayay ametoa kauli hiyo kutokana na sakata la muda sasa kati ya mchezaji huyo na mabosi wake hali iliyosababisha kuwa nje ya timu hiyo huku akiwa ametangaza kuvunja mkataba na klabu hiyo kabla ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuweka wazi kwamba bado ni mchezaji halali wa mabingwa watetezi hao wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mayay alisema sakata hilo linahitajika busara kubwa kutoka pande zote mbili ili kuweza kulimaliza kutokana na kila upande athirika.

“Nadhani jambo kubwa ni wao kuweza kutumia busara upande wa Yanga na wa Fei ili kuweza kumaliza hili jambo na kufanya mambo mengi yaweze kuendelea kwa sababu kinachotokea kwa sasa ni athari ambazo kila upande umekuwa ukizipata.

"Kila mmoja bado anahitaji kitu kutoka kwa mwenzake kwa sababu Yanga wao watakuwa waathirika kibiashara na wana mkosa mchezaji huyo," alisema Mayay.


Alisema pia mchezaji atakuwa anapata wakati mgumu kutokana na kukosa stahiki zake, lakini hata kipaji chake kwa kuwa muda mwingi amekuwa nje ya timu, hivyo bado wanayo nafasi wote kuweza kutumia busara kumaliza jambo hilo.

Hivi karibuni kiungo huyo alipeleka barua TFF kuomba kurejewa kesi yake katika Kamati ya Hadhi na Haki za Wachezaji ya shirikisho hilo.

Fei Toto ana mgogoro wa kimkataba na waajiri wake tangu mwishoni mwa mwaka jana baada ya kutumia kipengele kinachomtaka kurejesha fedha zake za usajili ili kuvunja mkataba, jambo ambalo waajiri wake walidai kuzirejesha kwa ni kinyume na utaratibu kimkataba.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad