Sallam Sk na Eric Omondi Watangaza Vita na Mandonga Mtu Kazi



Kupitia interview aliyofanya bondia mtanzania @k_mandonga iliyoruka kwenye ukurasa wa Instagram wa @bongofive ambayo Mandonga amewatemea mbovu mchekeshaji tokea nchini Kenya, @ericomondi na meneja wa wasanii tokea Record Label ya #wcb @sallam_sk , imewaibua wawili hao na kutaka pambano na Bondia huyo.


Kwenye post hiyo ya #bongofive , #sallamsk

Ameacha comment kuwa ushauri kwa Mandonga ulikuwa hauna maana mbaya, ila cha ajabu ni kuwa amekuwa akishambuliwa na Bondia huyo, Hivyo ametaka wadhamini wajitokeze kufadhili pambano kati yake na Mandonga huku akitishia kuja na ngumi aina ya DALUSO.


Kwa upande wa Omondi, yeye amechukua Clip ya Interview hiyo ambayo anazungumziwa na Mandonga na kupost kwenye ukurasa wake wa Instagram kisha kumtaka Bondia huyo kutojaribu moto wake, kutomzungumzia wala kumtaja maana atammaliza na kumkata mafuta aliyojaza kwa mwili.


Wawili hao, Kila mmoja kwa wakati wake, walimshauri Mandonga kutowasindikiza watu kwenye utajiri, bali ahakikishe kile anacho kifanya kinajaza hazina yake pia, kinyume na matarajio ya wengi, Mandonga amedai maoni ya wawili hao hayamaanishi uhalisia wao bali kila mmoja ameyatoa kutokana na sababu maalum, Kuhusu Omondi, Mandonga amedai pambano lake nchini Kenya lilifanya show ya mchekeshaji Omondi kubuma, na kuhusu Sallam, alimfanyia figisu kwenye mkataba wake na Wasafibet.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad