Serikali Kuwajadili Waliokacha Ukuu wa Wilaya




Wateule wa nafasi za Ukuu wa Wilaya ambao inasemekana wamekataa uteuzi huo watatakiwa kutoa maelezo ya kwa nini wameshindwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi kwa ajili ya uapisho.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama amesema wanasubiri taarifa kutoka kwa wizara zinazohusika ili waangalie taratibu na sheria zinasema nini juu ya viongozi wa Chama cha Walimu Nchini (CWT) kutotokea kula kiapo cha ukuu wa wilaya katika mikoa husika.

Viongozi walioshindwa kuapa ni Rais wa CWT, Leah Ulaya ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita na Katibu Mkuu wa chama hicho, Japheth Maganga aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Kagera

Katika kile kinachoonekana kutokuwepo kwa taarifa rasmi juu ya udhuru wao, Waziri Mhagama amesema yeye pia ameona kwenye vyombo vya habari kuwa wateule hao hawajaripoti katika viapo vyao kama walivyofanya wateule wengine katika maeneo yao ya kazi.

Amesema wateule hao walitakiwa kutii uteuzi huo kwa sababu katiba inamruhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Sululu Hassan kufanya hivyo.

Kumekuwa na mijadala katika mitandao ya kijamii kwa vigogo wa Chama cha Walimu Nchini (CWT) kutofika katika vituo vyao vya kazi kwa uapisho.

Amesema wanachosubiri ni taarifa rasmi kutoka wizara zinazohusika wao yaani Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad