Serikali yatoa Tamko Bungeni Sakatala la Viboko Shuleni



Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa
SERIKALI imewaagiza maafisa elimu wa mikoa na wilaya kuratibu usimamizi wa adhabu ya viboko shuleni, ili kuepusha vitendo vya walimu kutoa adhabu zinazoathiri wanafunzi, kinyume cha sheria na waraka namba 24 wa 2002, kuhusu muongozo wa utoaji adhabu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Agizo hilo limetolewa leo tarehe 2 Februari 2023 na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa, akizungumzia vitendo vya baadhi ya walimu kutoa adhabu kali kwa wanafunzi wanaofanya makosa shuleni.

“Natambua sio kusudio la walimu kuwadhuru wanafunzi, tukubaliane udhaifu wa uratibu wa usimamizi wa adhabu ya viboko shuleni. Nitoe wito kwa maafisa elimu mkoa na wilaya kuwakumbusha walimu wetu nchini kuzingatia muongozo wa utoaji adhabu shuleni chini ya kifungu cha 61 cha Sheria ya Elimu Sura 356, pamoja na kanuni zake,” amesema Waziri Majaliwa.


Waziri Majaliwa amesema kuwa, miongozo ya adhabu inasisitiza kwamba adhabu ya viboko itatolewa iwapo patatokea utovu wa nidhamu au kosa kubwa litakalofanywa ndani au nje ya shule na au itashusha heshima ya shule.


Katika hatua nyingine, Waziri Majaliwa amewataka wananchi kutosambaza video zinazoonyesha walimu wakitoa adhabu kwa wanafunzi ili kuzuia taharuki kwenye jamii, badala yake watu wanaotekeleza vitendo hivyo waripotiwe kwa mamlaka husika ili hatua zichukuliwe.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad