Simba Morali ipo Juu, Mastaa Wote Waingia Kambini Lazima Afe Mtu Kwa Mkapa

 


Kikosi cha Simba SC kimeingia kambini rasmi jana kujiandaa na mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca utakaopigwa Jumamosi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.


Baada ya kikosi kuwasili juzi alfajiri wachezaji walipewa mapumziko kutokana na uchovu wa safari.


Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo ambayo yamefanyika katika Viwanja vya Mo Arena chini ya kocha Roberto Oliviera ‘Robertinho’ na wasaidizi wake.


Morali ya wachezaji ipo juu na kila mmoja anaonekana kuhitaji kuaminiwa ili kupata nafasi katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Raja.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad