Simba Yaipiga Bao Newcastle, Yanga Timu Bora Duniani



Baada ya IFFHS kutoa orodha ya Ligi Bora duniani huku Ligi Kuu ya Tanzania ikiwa nafasi ya 39 duniani na ya tano (5) Afrika, kuna orodha pia ya klabu 502 bora duniani.

Kwa mujibu wa IFFHS wameangalia matokeo ya klabu na mafanikio iliyoyapata kwenye kipindi cha kati ya Januari hadi Disemba 31, 2022.

Kwa hiyo kwenye kila nchi wamepima matokeo na mafanikio ya kila timu halafu wanalinganisha na timu nyingine ili kupata orodha ya nafasi ya timu ya kwanza hadi mwisho.

Kwenye tatu (3) bora ya klabu bora duniani, nafasi ya kwanza na ya pili zipo klabu za Brazil ambazo ni Flamengo na Palmeiras halafu nafasi ya tatu ipo Liverpool ya England. Klabu nyingine kubwa duniani hazipo kwenye tatu bora!

Al Ahly ya Misri imeshika nafasi ya 17 kwenye orodha hiyo, kwa maana hiyo Al Ahly ni bora kwenye takwimu kuliko klabu kama Barcelona, Napoli, AS Roma, Arsenal n.k.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad