Stamina Asimulia Mkewe Alivyomkimbia na Kubeba Kila Kitu

 


Rapa Stamina, amesimulia jinsi alivyowahi kukutana na majanga ya kuuziwa gari la wizi na kujikuta yupo ndani, polisi Kijitonyama huku mke naye akiwa amemkimbia na vyombo vyake vyote.


Stamini alisimulia hayo alipokuwa akihojiwa kwenye kituo cha redio Clouds FM ambapo alisema, wakati huo aliyemsaidia alikuwa ni rafiki yake Roma na washkaji zake wengine kwani vinginevyo, msala ulikuwa mkubwa.


"Niliuziwa Harrier ya wizi, nakumbuka wakati huo nilikuwa nimeenda kwenye shoo sasa ile narudi nikakuta wife kabeba kila kitu kaondoka. Wakati natafakari hilo la mke wangu kubeba kila kitu, polisi wakaja kunikamata kwa ishu ya gari hilo la wizi. "Nilikaa ndani pale Mabatini Roma na washkaji zangu wengine wakaja kunipambania hadi nikatoka. Nikiwa polisi, kodi yangu ilikuwa imeisha. Mwenye nyumba naye akawa anataka chake na mimi sina kitu.


"Nilipotoka ikabidi nimuombe Roma niende kuishi Mbweni kwake huku vyombo vyangu nikivipeleka kwa bro kuvihifadhi. Aaliyekuja kuniokoa kwenye kipindi hicho, alikuwa ni dada mmoja ambaye nilikutana naye akanipa kampani ya kuingia studio nikaachia Asiwaze," anasema Stamina.


Stamina alisema, mwanamke huyo alimhifadhi kwa kuishi kwake na wakaanzisha mahusiano ya mapenzi na kufanikiwa kuzaa naye mtoto wake wa kwanza.


"Namshukuru sana huyo dada kwani ndiye niliyezaa naye mtoto wa kwanza. Alikuwa anakaa Tegeta, nilikuwa naenda Studio Kinondoni na kumbuka mimi staa siwezi kupanda daladala, yeye ndio akawa anasimamia shoo zote hizo bolt nauli na kula hata mavazi. Namshukuru sana, siko naye kwa sasa lakini tuko vizuri tunalea mtoto," alisema Stamina.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad