Tetemeko La Ardhi Uturuki: Mtoto Wa Miaka Mitano Aokolewa Baada Ya Saa 105 Kwenye Vifusi Vya Tetemeko

 


Mtoto mwenye umri wa miaka 5 ameokolewa kutoka vifusi vya tetemeko la ardhi la Uturki saa 105 baada ya mkasa huo .


Aras mwenye umri wa miaka mitano sasa ni mmoja wa miujiza ya Uturuki.


Vikosi vya uokoaji vilimtoa kutoka kwenye vifusi vya nyumba yake katika jiji lililoharibiwa la Kahramanmaras, saa 105 baada ya tetemeko la ardhi.


Alipofikishwa katika chumba cha wagonjwa mahututi, baridi kali ilikuwa imeingia na joto la mwili wake lilipungua hadi nyuzi 28 Selsiasi (digrii 82 Selsiasi).


Aras anaweza kuwa alinusurika, lakini dada yake mwenye umri wa miaka saba Hiranur hakunusurika. Wala kaka yake Alp mwenye umri wa miaka tisa hakutoka hain a baba yao pia aliaga dunia .


Ingawa sasa ana umri wa miaka 72, Mehmet babu yake , anatuambia kwamba kwa siku zake zote atamtunza Aras kana kwamba ni mtoto wake wa kiume.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad