Tetemeko Uturuki na Syria: Idadi ya Watu Waliofariki yafikia 9,504



Juhudi za uokozi wa watu waliokwama kwenye vifusi, zimeendelea nchini Uturuki na Syria baada ya tetemeko kubwa ambalo hadi hii leo Februari 8, 2023 vifo vimefikia zaidi ya watu 9,500 huku vikosi vya uokozi vikiendelea kuiondoa miili zaidi kutoka kwenye vifusi vya maelfu ya majengo yaliyoporomoka.


Kwa siku mbili mfululizo, tangu tetemeko hilo la kubwa la ardhi kutokea nchini Uturuki na Syria, vikosi vya uokozi vimekuwa vikifanya juhudi ya kuokoa watu katikati ya mazingira magumu huku waokoaji hao wakishangilia baada ya kumuokoa mtoto mchanga akiwa mzima wa afya.


Hadi sasa watu 6,957 wamefariki dunia nchini Uturuki na 2,547 Syria na kufanya idadi ya jumla kuwa 9,504, huku kukiwa na wasiwasi wa idadi hiyo kuongezeka mara mbili na zaidi ya watu 38,000 wamejeruhiwa.


Nchini Syria, serikali imesema inaendelea kuhamasisha uungaji wa mkono jitihada za kuwasaidia wahanga wa tetemeko hilo, ambazo hata hivyo imekiri zinaweza kuzuiwa na mzingiro wa magaidi na vizuizi vya magharibi.


Tayari Mataifa kadhaa, ikiwmo la Marekani, China na Mataifa ya Ghuba yameaanza kupeleka misaada ya kiutu na vikosi vya uokozi, wakati WHO ikikisia karibu watu milioni 23 huenda wameathiriwa na tetemeko hilo, na kutoa wito kwa mataifa kuharakisha zaidi juhudi za uokozi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad