Tito Amuandikia Rais Barua Kuhusu Jaji Biswalo


Baada ya Chama cha ACT-Wazalendo kutoa taarifa ya kuwataka Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) ambaye sasa ni Jaji wa Mahakama Kuu, Biswalo Mganga kujiulu, mawakili wa kujitegemea wamemwandikia barua Rais Samia Suluhu Hassan wakitaka Jaji Biswalo asimamishwe kazi.

Mawakili hao, Tito Elia Magoti na Peter Michael Madeleka wametoa mapendekezo mawili kwa Rais Samia moja likiwa kushauriana na Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma amsimamishe kazi Mganga ili kupisha uchunguzi.

Pendekezo lingine likiwa kuunda Baraza Maalum litakalochunguza na kupendekeza hatua stahiki dhidi ya Mganga ili kulinda utawala wa sheria na hadhi ya mahakama.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa Mganga alitumia vibaya matumizi ya ofisi na kusababisha ubadhilifu wa fedha za umma wakati akiendesha zoezi la ‘plea bargain’ zinazotolewa na makundi mbalimbali nchini ikiwemo wanasiasa, wanaharakati na waathirika wa zoezi hilo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad