TMA Yatabiri Mvua Kunyesha Mikoa Hii 16



Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa tatu usiku wa leo ikiitaja Mikoa 16 kukumbwa na mvua katika baadhi ya maeneo.

TMA imeitaja Mikoa itakayokua na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache pamoja na vipindi vya jua kuwa ni Kigoma, Katavi, Ruvuma, Tabora, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Geita, Songwe, Njombe, iringa, Mbeya, Rukwa na Kusini mwa Mkoa wa Morogoro.

Aidha, Mikoa ya Lindi na Mtwara itakua na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Maeneo ya Mikoa ya Dar es Salaam, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Dodoma, Singida, Visiwa vya Unguja na Pemba yanatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Kwingine ni Mikoa ya Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Mara, Simiyu, Tanga na Mkoa wa Pwani ukijumuisha visiwa vya Mafia.

Kwa viwango vya joto nchini, tazama hapa chini



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad