TMA Yatoa Tahadhari Upepo mkali, Mvua Maeneo Haya Leo Jumapili



Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Leo Februari 12 imetoa angalizo la kuwepo kwa upepo mkali kwa baadhi ya maeneo nchini huku maeneo mengine yakikabiliwa na mvua.

TMA imeyataja maeneo yatakayokuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache pamoja na vipindi vya jua kuwa ni Kusini mwa Mkoa wa Morogoro, Njombe na Iringa, Kigoma, Katavi, Ruvuma, Mtwara, Lindi, Songwe, Mbeya na Rukwa.

Mikoa ya Mara, Simiyu, Kagera, Geita, Mwanza na Shinyanga inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, ngurumo katika maeneo machache pamoja na vipindi vya jua.

Kwa upande wa Mikoa ya  Dar es salaam, Kaskazini mwa Morogoro, Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Tabora, Dodoma, Singida, Tanga, Mkoa wa Pwani ukijumuishwa na Visiwa vya Mafia pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba kunatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi pamoja na vipindi vya jua.

Katika hatua nyingine, TMA imetoa angalizo la upepo mkali unaofikia kilometa 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia Mita 2.0 katika maeneo ya Dar es Salaam pamoja, Visiwa vya Unguja na Pemba, baadhi ya maeneo ya Pwani ya Kaskazini ya Bahari ya Hindi (Tanga) na Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia.

Kwa taarifa zaidi na viwango vya joto nchini, tazama hapa chini.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad