Uchaguzi Wa Nigeria 2023: Upinzani Wasusia Matokeo Yaliyoanza Kutangazwa

 


Vyama vya upinzani vimetoka nje ya ukumbi ambapo matokeo ya uchaguzi wa rais wa Nigeria wenye upinzani mkali yanatangazwa.


Chama kikuu cha upinzani cha Peoples Democratic Party (PDP) na Labour Party vimedai hakuna uwazi katika mfumo mpya wa kielektroniki wa wapiga kura.


Huu ni uchaguzi wa kwanza wa kitaifa ambapo kifaa cha kielektroniki kimetumika kuwaidhinisha wapiga kura.


Tume ya uchaguzi imekanusha malalamiko ya vyama vya upinzani.


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (Inic) Mahmood Yakubu alisema utangazaji wa matokeo utaendelea.


Mwakilishi wa PDP katika kituo cha uchaguzi huko Abuja alielezea mchakato huo kuwa wa udanganyifu, na kushutumu chama tawala cha All Progressives Congress (APC) kwa kushirikiana na IEC, huku chama cha Labour kikiomba kusitishwa kwa matangazo hayo, au uchaguzi kufutwa na kurudiwa upya.


Chama cha APC ambacho mgombea wake Bola Tinubu amepata uongozi wa mapema kutokana na matokeo yaliyotangazwa kufikia sasa, kimesema kwamba wale ambao hawajaridhika na matokeo hayo waende mahakamani, na vyama hivyo viache kwanza mchakato huo uendelee.


Huku takriban thuluthi moja kati ya majimbo 36 yakitangazwa rasmi, Bw Tinubu ana asilimia 44 ya kura zilizopigwa, mbele ya Bw Abubakar kwa 33%, na Bw Obi kwa 18%.


Hata hivyo, matokeo mengi ambayo bado yanatoka kaskazini na kusini-mashariki, yanayoonekana kama ngome za PDP na Labour Party mtawalia, hivyo matokeo ya mwisho bado hayatabiriki.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad