Ufafanuzi Ukarabati wa Kivuko cha MV Magogoni Kutumia Bilioni 7.5



Meneja wa Vivuko Kanda ya Mashariki na Kusini, Mhandisi Lukombe King’ombe ametolea ufafanuzi juu ya bei ya ukarabati wa Kivuko cha MV Magogoni kufuatia kuibuka kwa mjadala mtandaoni baada ya gharama za ukarabati huo kutajwa kuwa ni Tsh. Bilioni 7.5 na wengine kusema ni kubwa na wakitaka kujua bei ya kivuko kipya.


“Kivuko hiki ni kweli kimejengwa kwa Bilioni 8.5 mwaka 2008 lakini fedha ya wakati ule thamani yake haifanani na mwaka huu, na kinatakiwa kufanya kazi kwa miaka 30 na ndio kwanza kina miaka 15 tangu kijengwe, sio sawa kukiacha bila kukarabati na kununua kipya”


“Tsh. Bilioni 7.5 hatujapigwa vifaa vya majini vina bei kubwa, Mkandarasi atabadili kabisa engine na gia box zake ambazo ni 4 na ataweka mpya pamoja na moja ya tano ya akiba, vitu vya majini ni bei kubwa gear box moja tu ni sawa na kununua Prado TX mpya, engine na gear box moja tu ni USD Elfu 90, bado atanunua vifaa vipya vya kujiokolea”


“Kuhusu wanaohoji kwanini hatujampa Mkandarasi Mzawa Songoro yeye alitaka akarabati kwa zaidi ya Tsh.Bilioni 10 , kwa wanaouliza kwanini hatujanunua kivuko kipya thamani ya kivuko kipya kama hiki cha MV Magogoni sio chini ya Tsh. Bilioni 25”


Itakumbukwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa juzi aliitaka Kampuni ya Afrika Marine and General Engineering ya Mombasa, Kenya kukarabati kwa wakati kivuko hicho ndani ya miezi mitano kama mkataba unavyosema, kivuko hicho kitapelekwa Mombasa kwa ukarabati hivi karibuni.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad