Ukiwekewa Puto Tumboni Huruhusiwi Kunywa Pombe be


Moja kati ya habari kubwa tulizoanza nazo mwaka huu ni huduma ya kuwekewa puto tumboni kwa ajili ya kupunguza uzito ambayo inatolewa Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila na tayari Mwimbaji Peter Msechu @peter_msechu amebainisha kupungua kilo saba, siku 7 tu baada ya kuwekewa puto katika Hospitali hiyo ili kumsaidia kupunguza uzito mwilini mwake.

@ayotv_ imefika hadi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili - Mloganzila na kupata fursa ya kuona Mtu akiwekewa puto pamoja na kuongea na Madaktari ambao wameelezea mengi tusiyoyafahamu kuhusu huduma hiyo.

“Gharama za kuwekewa puto ni Tsh. Milioni 4.2 na tayari tumeshawawekea Watu 34 wakiwemo Watu maarufu ambao wengine hawajataka kujitangaza”

Madaktari wanasema ukiwekewa puto likiwa tumboni unaweza kufanya mazoezi na sarakasi nyingine zozote ila hautoruhusiwa kunywa bia na soda kwakuwa ukinywa vinaathiri puto na linaweza kupasuka… kuitazama video hii kwa urefu ingia

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad