Unaambiwa Yanga Imevuta Milioni 33 Kutoka Kwa Viongozi Mbali Mbali, Eng. Hers Afunguka




Rais wa Klabu ya Yanga Eng. Hersi Ally Said @caamil_88 amekiri kupokea Shilingi Milioni 15 kutoka kwa Mhe.Rais Samia Suluhu Hasaan, alizoahidi kununua magoli yatakayofungwa kwenye mchezo wao dhidi ya TP Mazembe , lakini pia Viongozi mbali mbali wameunga mkono kwa kununua kila goli moja kwa Milioni 1 na kufanya Jumla kuwa Milioni 33.


Viongozi waliotoa zawadi ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara , Waziri wa fedha , Waziri wa Sanaa na Michezo, Waziri wa Utalii , Naibu Waziri wa Ardhi, Mwenyekiti wa DRFA ( Hawa wote wametoa Milioni 1 kwa kila goli) fedha zote zitapokelewa na watapewa Wachezaji na Benchi la Ufundi amesema Rais wa Klabu ya Yanga kwenye #LeoTena ya CloudsFM.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad