Unyama! Binti Adaiwa Kumchinja Mama yake Akimtuhumu Kumuua Mwanae

 


Juma Charles na mke wake Joyce Julius, wakazi wa kijiji cha Bunegezi Wilaya ya Geita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kushirikiana kumuua mama mkwe wake Butamo Igenzelo (70) kwa imani za kishirikiana.


Habari zilizopatikana kutoka kijiji cha Bunegezi na kuthibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Berthaneema Mlay zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi Alhamisi Februari 22, 2023.


Akizungumza jana Ijumaa Februari 24, 2023, Kaimu kamanda huyo amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu Butamo ambaye ni mama mzazi wa Joyce aliuawawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni.


“Bibi huyu alikatwa na kitu chenye ncha kali shingoni na kupoteza maisha kwa kuvuja damu nyingi; mwili wake umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Geita,” amesema kaimu Kamanda huyo


Amesema mauaji hayo yametokea wiki moja baada ya kifo cha mtoto wao ambapo bibi yake ambaye sasa pia ni marehemu alituhumiwa kuhusika na kifo hicho kwa imani za kishirikina.


Akizungumzia matukio ya mauaji yanayohusiana na imani za kishirikina, Juliana Maduhu, mkazi wa mtaa wa Igogo jijini Mwanza ameishauri jamii kuacha imani potofu zinazosababisha chuki, uhasama na mauaji.


“Ni jambo linalosababisha laana katika jamii watoto kuwauwa wazazi au wazazi kuwauwa watoto wao kwa imani za kishirikina. Nawaomba viongozi wa dini waongeze mafundisho ya kiimani kutokomeza vitendo hivi katika jamii,” amesema Juliana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad