Utalipa 28,000 Kwa Mwezi ili Kupata Instagram Verification


 Meta imetangaza itaanza kuweka huduma ya kulipia ili kuweza kupata verification.

Huduma hii itakuwa inafanana na Twitter Blue; watumiaji wataweza kulipia ili kupata alama ya verification na upendeleo wa akaunti kuwa tofauti. Instagram na Facebook zitaendelea kupatikana bure, lakini kwa ambao watahitaji Badge ya verification watalipia.


𝗪𝗮𝘁𝘂𝗺𝗶𝗮𝗷𝗶 𝘄𝗮𝗸𝗶𝗹𝗶𝗽𝗶𝗮 𝘄𝗮𝘁𝗮𝗸𝘂𝘄𝗮 𝘄𝗮𝗻𝗮𝗽𝗮𝘁𝗮:

🔘 Badge ya verification

🔘 Meta itazuia mtu asifungue akaunti kama yako au akaunti za kutumia majina yako

🔘 Meta itaweka support ya huduma kwa wateja

🔘 Comments yako itaonekana kwa urahisi

🔘 Utapata upendeleo wa content zako kuonekana kwenye page ya Explore, Search na Reels

🔘 Utapata Stickers maalum kwenye IG Stories.

🔘 Akaunti ambayo imelipia verification itakuwa ya mwanzo kuanza kupata mabadiliko mapya kabla hayajaanza kutoka kwa watumiaji wote.

Meta imesema gharama zake zitaanza kuwa Dola 11.99 (sawa na Tshs 29,000 kwa mwezi) endapo kama utajiunga kwa kutumia Website. Kama utajiunga kwa iOS utalipia 14.99 (sawa na 35,000 TZS) kwa mwezi (gharama ambayo imeongezeka ni gharama ya asilimia ya Apple).

Twitter, Snapchat, na Telegram ni moja kati ya apps ambazo zinatumia utaratibu huu!

Je unadhani mitandao kuanza kulipisha watumiaji wake ili kupata huduma za kipekee na verification ni sawa?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad