Wafanyakazi TRA Wakamatwa na Polisi Iringa

 


Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa linawashikilia Wafanyakazi wa TRA, Upendo Msigwa mwenye umri wa miaka 32 Mkazi wa Mawelewele na Chali Chaliga mwenye umri wa miaka 28 Mkazi wa Donbosco kwa kosa la kutoa leseni bila kufuata sheria na taratibu za Nchi zinavyotaka.


Akiongea na Waandishi wa Habari wa Iringa, RPC wa Iringa, Allan Bukumbi amesema Wafanyakazi hao wa TRA wamefanya kazi kinyume na sheria hivyo Jeshi la Polisi linawashikilia na upelelezi ukikamilika watafikishwa Mahakamani.


Kamanda Bukumbi amesema Jeshi la Polisi liliwakamata Omary Kibao (38), Johnson Kihongosi (31), Dickson Nelson(32) kukutwa na leseni za udereva 31, vitambulisho vya NIDA na Mpiga kura 04, nakala za magari ya Watu mbalimbali na Police loss report.


Aidha Kamanda Bukumbi amesema kuwa Watuhumiwa hao walikuwatwa na namba za magari na Pikipiki 431, TIN numbers 08, printer 05, laptop 1 na desktop 1, nakala za vyeti vya mafunzo ya udereva 02, scaner 01 na lamination mashine 1.


Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kwa ushirikiano na Askari wa Uhifadhi kutoka Hifadhi ya Taifa Ruaha wamefanikiwa kumkamata Madambo Nyambinga miaka 27 baada ya kukutwa na silaha moja aina Gobore iliyotengenezwa kienyeji ikiwa imehifadhiwa ndani ya gogo pori la Liyangoro lililopo Kijiji cha Idodi na Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani upelelezi ukikamilika.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad