Wakazi Apingana na Babu Tale Kuhusu Ukubwa wa Wimbo wa Zuwena


Rapper Wakazi apingana na kauli ya Babu Tale kwamba wimbo #Zuwena wa mwanamuziki Diamond Platnumz umekuwa wimbo mkubwa Afrika.


Wakazi ameipigilia msumali kauli yake hiyo akieleza wimbo huo ni mkubwa Afrika Mashariki tu na sio Afrika nzima kwa sababu haupo kwenye Top 20 za nchi kama Nigeria, Ghana, Congo, South Africa n.k

""Oya ni Mkubwa Africa huu eti? 😁.. Nadhani ni mkubwa Africa Mashariki tu. Sema wimbo mzuri. haupo top 20 za other big african markets (Nigeria, Ghana, Congo, South Africa, etc) na nadhani tunahitaji hujui why? Tupate muda tuyajenge haya Babutale" - ameeleza Wakazi.


Hayo yameelezwa na Wakazi kwenye sehemu ya komenti katika posti ya Babu Tale ambayo alikuwa anawavunjia mashabiki wasiyoyajua mashabiki kuhusu wimbo huo akiutaja uliorekodiwa miaka minne iliyopita, ambapo yeye na viongozi wengine wa WCB walishaukatia tamaa ya kwamba hautatoka lakini Diamond aliona huu ndio wakati wa kazi hiyo kutoka na kazi hiyo inafanya vizuri zaidi.

Aidha, wimbo #Zuwema unaendelea kufanya vizuri maeneo mbalimbali ukiwa upo kwenye Trending kwenye nchi zaidi ya 9 Duniani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad