Waliokufa na Tetemeko Wafikia 25,000

 


Hali mbaya ya usalama kusini mwa Uturuki imevuruga juhudi za uokoaji kufuatia tetemeko baya la ardhi lililotokea Jumatatu, makundi ya kimataifa yamesema.


Wafanyakazi wa uokozi wa Ujerumani na jeshi la Austria walisitisha shughuli zao za utafutaji, wakitaja mapigano kati ya makundi ambayo hayakutajwa.


Pia kumekuwa na ripoti za uporaji. Rais wa Uturuki amesema atatumia mamlaka ya dharura kumuadhibu yeyote atakayevunja sheria.


Idadi ya vifo kutokana na tetemeko la ardhi sasa imepindukia 25,000 na matumaini yanafifia ya kupata manusura wengi zaidi chini ya vifusi, licha ya visa vya uokoaji wa miujiza.


Kulikuwa na ripoti mapema Jumamosi kwamba mapigano kati ya makundi yasiyojulikana katika jimbo la Hatay yamewaacha wafanyakazi kadhaa kutoka Kitengo cha Misaada ya Maafa cha Vikosi vya Austria wakitafuta hifadhi katika kambi ya msingi na mashirika mengine ya kimataifa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad