Wanigeria wameikamata dunia, Burna boy, Rema na Tems kutumbuiza NBA ALL STAR

 


February 19 huko Salt Lake City, Utah nchini Marekani kutakuwa na tukio kubwa la mpira wa kikapu ambalo linajulikana kama NBA All-Stars’ kutakuwa na mchezo wa NBA ALL STAR.


Katika tukio hilo shirikisho la mpira wa kikapu nchini Marekani limetangaza kuwa  Wasanii kutoka Nigeria barani Africa ambao ni Tems, Burna Boy na Rema wametatumbuiza kwenye half time show tarehe 19 Februari 2023 kwa mara ya kwanza kwa uapnde wao.


Hii ni kwa mara ya kwanza kwa wasanii kutoka barani Afrika kutoa burudani kwenye tukio hilo kubwa na la kihistoria nchini Marekani.


Wasanii kutoka Nigeria wamekuwa wakitajwa kwenye matukio makubwa sana duniani.


Hii inaleta picha kuwa kwa sasa wasanii kutoka nchini Nigeria wamekuwa wakifuatiliwa sana duniani na muziki wao umeikamata dunia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad