Yanga Afrika Yachimba Mkwala Mzito CAF



Uongozi wa Klabu ya Young African umewashuka Presha Mashabiki na Wanachama wake, kwa kuweka wazi mipango na mikakati ya kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika Hatua ya Makundi.

Young Africans itaanzia ugenini mjini Tunis-Tunisia kucheza na US Monastir Jumapili (Februari 12), huku ikitambia Rekodi yake ya kushinda nchini humo, kwa kuifunga Club Africain kwenye mchezo wa hatua ya Mtoano.

Afisa Habari wa Young Africans Ally Kamwe amesema: “Tumekuwa kimya sana kuhusu maandalizi yetu ya mashindano ya Kimataifa, hii ni kwa sababu kuna mambo mengi, hivyo kila kitu kinafanyika kimya kimya, lakini niwahakikishie kuwa tumeshakamilisha kwa asilimia kubwa maandalizi yetu.”

“Mchezo wetu dhidi ya US Monastir unatarajiwa kucheza nchini Tunisia ambapo tumekuwa na Rekodi nzuri ya kushinda dhidi ya Club Africain kwenye hatua ya mtoano, na sasa tunataka kwenda kuandika Rekodi nyingine ya ushindi ili kuanza vizuri hatua ya Makundi.”

“Tuna Benchi zuri la Ufundi na Wachezaji imara na wenye uwezo wa kupambana popote katika bara hili la Afrika, hapa ninawazungumzia akina Fiston Mayele, Khalid Aucho, Mudathir Yahya na wengine, hawa wote wanajua kazi ni kubwa na ngumu lakini wanatambua tunahitaji alama tatu ugenini na nyumbani.”

Baada ya mchezo dhidi ya US Monastir, Young Africans itarejea nyumbani Dar es salaam kucheza dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo Februari 19, kisha itakwenda nchini Mali kuikabili Real Bamako, katika Uwanja wa du 26 Mars, mjini Bamako Februari 26.

Machi 08, Young Africans itacheza Mchezo wa Mzunguuko wa Nne wa Kundi D dhidi ya Real Bamako Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, Kabla ya kuikaribisha US Monastir Machi 19. Wananchi watamalizia ugenini kwa kukabili TP Mazembe mjini Lubumbashi katika Uwanja wa TP Mazembe, April 02.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad