Ofisa Habri wa Klabu ya Young Africans, Ali Kamwe amewataka mashabiki wa timu hiyo kuacha kuwa wanyonge kisa wamefungwa na US Monastir kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika nchini Tunisia.
Kamwe amesema kuwa hakuan hata timu moja iliyopata matokeo ya ushindi ugenini kati ya michezo nane ya Kombe la Shirikisho iliyochezwa wikiend hii hivyo hawapaswi kuwa wanyonge na kuwataka waachane na takwimu za mitandao ya kijamii.
”Niwaambie mashabiki na wanachama wa Young Africans, kila mmoja ameumizwa na matokeo, sio matokeo ambayo tumekuwa tumejiandaa nayo kuyapokea, kila mmoja amekuwa amejiandaa kupata matokeo ya ushindi kwenye ardhi ya ugenini.
”Niwaambie mashabiki na wanachama wa Young Africans, tusiwe wanyonge, tusifikiri kwamba tumepoteza kitu kikubwa, ule haukuwa mchezo wa mwisho wa makundi, ulikuwa mchezo wa kwanza kwa hatua ya makundi.”
”Naomba niwaambie kitu, ukiangalia kwenye Kombe la Shirikisho ndo kumechezwa michezo nane, kwenye michezo hiyo yote hakuna timu imeweza kushinda kwenye uwanja wa ugenini Kombe la Shirikisho, ni timu tatu tu ndiyo zimeweza kupata sare kwenye viwanja vya ugenini. Maana yake timu tano zimekuwa nyumbani zote zimeshinda, tatu zilizokwenda ugenini zimeweza kupata sare.”
”Hii michezo ya Afrika kuanzia Ligi ya Mabingwa na Shirikisho kila mtu amejihimarisha kwenye ardhi yake ya nyumba, kila mtu anataka kuwa bora na kuokota na alama tatu kwenye mchezo wake wa nyumbani kwa hiyo sisi Young Africans hatutakiwi kuweka vichwa chini, tusiweke vichwa vyetu chini tuachane na hizi chambuzi za kwenye ma-group ya ‘WhatsApp’. tuachane na chambuzi za mitandao ya kijamii.”
Imeandikwa na @fumo255