Zuchu amtaka mumewe asiwe na tarajio la makalio makubwa


Malkia wa Bongo Zuhura Othman almaarufu Zuchu amemuonya mume wake mtarajiwa asiwe na matarajio makubwa juu yake.

Kwenye akaunti yake ya mtandao wa Snap chat, msanii huyo wa WCB alibainisha kuwa huenda mume wake mtarajiwa, popote alipo, anaweza kuwa na matarajio mengi makubwa kuhusu mwonekano wake.

Hata hivyo, alimtaka mwanaume huyo ajue kuwa makalio yake si makubwa kama jinsi wanaume wengi wanapendelea.


"Mpendwa mume wangu mtarajiwa, najua huko ulipo una matarajio makubwa sana juu ya mwonekano wangu, ila naomba nikuondolee tarajio moja, sina traako mpenzi😂😂😂😂😂," Zuchu aliandika. 

Mara nyingi, Zuchu hutumia akaunti zake za mitandao ya kijamii kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusu maisha yake, kuanzia hisia, masuala mahusiano, muziki, hisia na mengineyo.

Kwa muda mrefu, mwimbaji huyo kutoka Zanzibar amekuwa akidaiwa kuwa kwenye mahusiano na bosi wake Diamond Platnumz.

Wiki chache zilizopita hata hivyo, mamake Zuchu, Khadija Kopa alisisitiza kuwa bintiye yuko single kwani bado hajachumbiwa.


Kulingana na malkia huyo wa mipasho ya Taarab, bintiye hachumbiani na msanii Diamond kama ambavyo wengi wamekuwa wakiaminishwa kwa muda mrefu wa zaidi ya mwaka mmoja na miezi kadhaa sasa.

Kopa alisema kuwa kutokana na umaarufu wa Zuchu, siku akipata mchumba dunia nzima itajua na itakuwa ni habari ya mijini na vijijini, ila kwa sasa akawataka watu kuwa na subira na kutopotoshwa na kile ambacho wamekuwa wakikisikia mitandoani na kwenye mablogu ya udaku.

“Zuchu bado yupo single, hana Mpenzi wala Mchumba na wala hajanitambulisha kwa Mwanaume yoyote kwamba Mama huyu ndiye Mwanaume wangu, Zuchu ni maarufu hata mimi Mama yake ni maarufu siku atakapopata Mchumba akanitambulisha matajua tu muwe na subira,”  alisema Khadija Kopa.

Mwaka jana, Zuchu na Diamond walidokeza kuwa kuna kitu kinachoendelea kati yao kutokana na matendo yao pamoja. Wawili hao walionekana wakijivinjari, kudensi pamoja, kuzawadiana na hata kubusus hadharani

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad