Zumaridi Afichua Ugonjwa Alioumwa Gerezani "Nilitengwa na Wafugwa Wenzangu"

 


Mwanza. Mhubiri, Diana Bundala maarufu "Mfalme Zumaridi" amefunguka magumu aliyopitia akiwa gerezani kuwa ni pamoja na kuugua ugonjwa wa shinikizo la damu 'presha' ambao hakuwa nao, huku akitengwa na baadhi ya wafungwa wenzake.


Zumaridi ametoa kauli hiyo leo nyumbani kwake baada ya kumaliza kifungo chake cha mwaka mmoja katika Gereza la Butimba jijini Mwanza baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza kumtia hatiani katika shtaka la kuzuia maofisa wa serikali kutekeleza majukumu yao.


Amesema hatasahau miezi 10 ya mwanzo kati ya 11 aliyokaa ndani ya gereza hilo tangu alipokamatwa kutokana na baadhi ya wafungwa kumtenga jambo lililomnyima amani ndani ya gereza hilo.


RELATED

Mfalme Zumaridi arejea uraiani, waumini wampokea kwa staili yao

Kitaifa 10 hours ago

Zumaridi asimulia mahabusu walivyomkimbia

Kitaifa 10 hours ago

"Maisha ya gerezani ni changamoto kwa sababu unakuwa chini ya ulinzi, sikuwa na amani yoyote. Niliishi kwa mateso mpaka nimepata presha, nilikuwa kawaida lakini baada ya kuingia gerezani nimepatwa ugonjwa huo," amesema.


 "Nilitengwa na watu wote, wafungwa wenzangu na watu wangu niliyoingia nao gerezani walizuiwa kunisogelea, mule ndani ya gereza la wanawake kuna mwembe niliambiwa nikae kwenye mwembe peke yangu kwa hiyo sikuwa na sehemu ya kukimbilia," ameongeza


Mhubiri huyo amesema alianza kupata amani Oktoba mwaka jana baada ya uongozi wa gereza hilo kubadilishwa, ambapo mkuu wa gereza hilo aliletwa mpya ambaye alikuwa akisikiliza kero na maoni ya wafungwa katika gereza hilo.


Ameiomba serikali na Rais Samia Suluhu Hassan kufanya ufuatiliaji wa kina ndani ya magereza nchini ili kubaini madhaifu yaliyomo na kuepusha ukiukwaji wa haki za wafungwa.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad