Ahmed Ally "Hamasa inahamia dhidi ya Horoya Tuipeleke Simba Robo Fainali"

 




Meneja wa Habari na Mawasilino Simba SC Ahmed Ally ametangaza rasmi kuzifunga sherehe za ushindi wa mchezo wa Mzunguko wanne wa Kundi C, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Vipers SC.


Simba SC ilichomoza na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mabingwa hao wa Uganda juzi Jumanne (Machi 07), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, bao likifungwa na kiungo kutoka nchini Zambia Clatous Chotta Chama.


Ahmed ametumia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii kutoa taarifa za kufungwa kwa sherehe za ushindi huo, huku akithibitisha kufunguliwa kwa mlango wa hamasa ya mchezo wa Mzunguko wa tano dhidi ya Horoya AC ya Guinea, utakaopigwa Jumamosi (Machi 18), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.


Mechi yetu na Horoya ni Jumamosi Marchi 18 saa 1:00 Usiku tukishinda mchezo huo moja kwa moja tunatinga Robo Fainali.


Maandalizi ya kiufundi tuwaachie wataalamu, Sisi mashabiki tuanze maandalizi yetu ya kuujaza Benjamini Mkapa.


Kila mwana Simba ana wajibu wa kuisaidia Simba kutinga Robo Fainali msimu huu


Nabi atetea maamuzi ya kumtoa Aziz KiHamasa zianze sasa kwenye Matawi, Mitaaa, Masoko pamoja na Makundi yetu ya wastup kuhakikisha kwamba hakuna Mwana Simba anabaki nyumbani siku iyo.


Mpango wa hamasa kitaifa tutautangaza punde tuu baada ya mechi ya Mtibwa Sugar


Tuungane pamoja kuipeleka Simba Robo Fainali.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad