Anayedaiwa Kumuua Mkewe na Kumchoma Kwa Magunia Ya Mkaa Aomba Aachiwe Huru






Mfanyabiashara Khamis Luwonga (38) anayetuhumiwa kumuua mke wake na kisha kuchoma mwili wake kwa magunia ya Mkaa, aneiomba mahakama imuachie huru kwa sababu mpaka sasa hakuna ushahidi wa kutosha kumshtaki.

Luoga anayekabiliwa na kesi ya mauaji namba 5, 2022 iliyoko katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, amewasilisha ombi lake hilo mbele ya Jaji Bwagoge wa

Mahakama Kuu Masijala Kuu kupitia wakili wake, Mohamed Majaliwa akidai kuwa kesi iliyopo Kisutu inamapungufu kisheria.

Akiwasilisha hoja zake mbele ya Jaji Bwagonge, Majaliwa amedai kuwa, mteja wake (Luoga) anashtakiwa kwa kosa la mauji mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Rhoda Ngimilanga wa Mahakama ya Kisutu na kwamba kesi hiyo inaonekana mpya lakini kiuhalisia sio mpya kwa sababu kesi ya mauji namba 4,2019 dhidi ya mteja wake ilikwisha kumalizika.


Amedai mashtaka yaliyokuwepo kwenye hati hiyo yalipitia hatua zote za kisheria na Oktoba 24,2022 kesi iliitwa mahakamani kwa ajili ya kusikilizwa ambapo upande wa mashtaka ulidai kuwa na mashahidi wanne.

Amedai kuwa, wakili wa Serikali Mwandamizi, Mwasiti Ally alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga wa Mahakama ya Kisutu kuwa kesi iliitwa kwa ajili kusikilizwa, lakini Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya mshtakiwa.


Majaliwa akadai kutokana na kuomba kuondolewa kwa kesi hiyo, Hakimu Ruboroga alimuachia Luwonga, lakini cha kushangaza mshtakiwa alikamatwa tena na askari na baada ya saa chache baadae alipandishwa tena kizimbani na kusomewa mashitaka yale yale mbele ya Hakimu Ngimilanga


Baada ya Jaji kusikiliza hoja za pande zote mbili ameahirisha maombi hayo hadi Aprili 18, 2023 kwa ajili ya uamuzi. Mshtakiwa Luwoga anatetewa na wakili, Majaliwa Zidadi Mikidadi na Fatuma Abdul

Luwonga amefungua maombi Mahakama Kuu ili wapate maelezo ya uhalali wa kesi namba 5,2022 ya mauji baada ya kesi ya halali dhidi yake kufutwa na kufunguliwa upya.

Katika kesi hiyo ya muaji namba nne ya mwaka 2019, mshitakiwa Luwonga ambaye ni Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam

Katika kesi hiyo inadaiwa, Mei 15, 2019 huko Gezaulole eneo la Kigamboni mshtakiwa Luwoga anayeishi Kigamboni jijini Dar es Salaam, alimuua Naomi Marijani na kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya Mkaa ambapo alichukua majivu ya marehemu na kwenda kuyafukia shambani kwake.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad