Baada ya utafiti wa miaka mitatu mnyama huyu atajwa kuwa chanzo cha Corona




Sasa tunaweza kusema dunia ina "ushahidi bora" zaidi ambao tunaweza kujua jinsi virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 viliambukizwa kwa mwanadamu kwa mara ya kwanza, timu ya wanasayansi imedai.

Ni mabadiliko ya hivi punde ya kisayansi katika utafutaji wa chanzo, ulio na siasa nyingi kwa sababu ya janga hili mbaya zaidi katika karne moja, ambao umetoa nadharia kadhaa zinazoshindana na kupishana ambazo hazijathibitishwa au kukanushwa kabisa.

Uchanganuzi wa hivi majuzi zaidi unaashiria spishi fulani ya wanyama kama chanzo cha virusi vya Corona. Uchambuzi huo unatokana na ushahidi ambao ulikusanywa miaka mitatu iliyopita kutoka Soko la Wanyamapori la Huanan huko Wuhan, ambalo limekuwa kitovu cha mlipuko wa awali.

Katika siku za mwanzo za 2020, wakati Covid bado ilikuwa ugonjwa wa kushangaza, Vituo vya Udhibiti wa Magonjwa vya Uchina (CDC) vilichukua sampuli kutoka sokoni.

Taarifa za kinasaba zilizomo katika sampuli hizo zimetolewa hivi majuzi, kwa ufupi, hadharani, na hiyo iliwezesha timu ya watafiti kuzichambua na kueleza mbwa wadogo wanaofahamika kama racoon dogs ndio chanzo cha kusambaza ugonjwa huo kwa watu.

Kiini cha uchambuzi huu ni kwamba vinasaba (DNA) kutoka kwa mbwa hawa, wanyama wa mwituni ambao walikuwa wakiuzwa moja kwa moja kwenye masoko ya nyama vilipatikana na pia kwenye vifaa na matambara ya kupigia deki sokoni ambayo yalipatikana na SARS CoV-2, kulingana na uchambuzi ambao ilichapishwa mtandaoni tarehe 

Lakini katika utafutaji kiini cha mlipuko huo wa Covid-19, ambapo soko limefungwa kwa muda mrefu na wanyama waliokuwa wanauzwa kuuawa, bado hatuna uthibitisho wa uhakika. Na kucheleweshwa kwa miaka mitatu katika kutoa ushahidi ama data hii muhimu kumeelezewa na wanasayansi wengine kama "kashfa".

Matokeo hayo yamechapishwa huku kukiwa na ishara kwamba nadharia ya uvujaji wa maabara inazidi kupata msingi miongoni mwa mamlaka nchini Marekani.

Serikali ya China imekanusha vikali maoni kwamba virusi hivyo vilitoka katika kituo cha kisayansi, lakini FBI sasa wanaamini kuwa hali hiyo ndiyo "uwezekano mkubwa", kama inavyoamini Idara ya Nishati ya Marekani.

BBC imezungumza na baadhi ya wanasayansi waliohusika katika misheni ya miaka mitatu ya kuchunguza asili ya Covid. Wanaamini kuwa uchambuzi huu mpya unaweza kuwa wa karibu zaidi kupata kuelewa jinsi milipuko hiyo ilivyoanza, na kwamba utofauti wa mtazamo kati ya China na Magharibi unazuia juhudi za kisayansi za kutatua siri hiyo.

Utafiti mpya unaonyesha nini?
Dk Florence Debarre, mtafiti mkuu katika Taasisi ya Ikolojia na Sayansi ya Mazingira huko Paris, amekuwa sehemu muhimu ya utafiti huu. Aliiambia BBC kwamba alikuwa "ameshangazwa" na kutafuta data hii tangu alipogundua kuwa ipo.

"Tuliona matokeo yakionekana kwenye skrini zetu, na ilikuwa: mbwa, mbwa wa racoon, mbwa wa racoon," alikumbuka.

"Kwa hivyo tuligundua wanyama na virusi [kwa pamoja]," alielezea Dk Debarre. "Hiyo haithibitishi kuwa wanyama waliambukizwa, lakini hiyo ndiyo tafsiri inayokubalika zaidi ya kile tumekiona."



Kwa mujibu wa Prof Eddie Holmes kutoka Chuo Kikuu cha Sydney, ambaye pia alihusika katika utafiti huo, huu ni "ushahidi bora kusaidia kupata" asili ya mnyama aliyesababisha virusi.

"Hatutawahi kupata mnyama aliyetumika (kusambaza virusi) - ametoweka," Prof Holmes aliambia BBC.

"Lakini ni ajabu kwamba data ya kinasaba imegundua wanyama hawa - na inatuambia sio tu ni viumbe gani vilivyokuwepo, lakini ni wapi walikuwepo- sokoni," Prof Holmes aliambia BBC.

Wanasayansi wanaweza kufanya nini sasa ili kupata asili ya Covid?
Data hii mpya inaweza kutoa miongozo zaidi kwa uchunguzi zaidi juu ya chanzo cha mlipuko huo, lakini kufuata miongozo hiyo itakuwa ngumu.

Prof Marion Koopmans kutoka Chuo Kikuu cha Erasmus huko Rotterdam alikuwa sehemu ya timu ya uchunguzi ya Shirika la Afya Ulimwenguni iliyokwenda Wuhan mnamo 2020. Alieleza kwamba uchambuzi huo mpya "uliweka uwepo wao kwenye vibanda maalum, ili kuangalia ni wapi wanyama wanaouzwa huko walitoka" .

"Bila shaka kama hiyo ni sehemu ya mauzo haramu, swali ni kama utaweza kujua hilo."

Bado kunaweza kuwa na ushahidi wa kibaolojia katika mashamba ambapo wanyama hawa wanafugwa kwa ajili ya biashara. Ikiwa watafiti wangeweza kupata wanyama wanaofugwa na kingamwili zinazoonyesha walikuwa wameambukizwa SARS Cov-2, hiyo inaweza kutoa kidokezo kingine.

Lakini kupata virusi halisi katika mnyama, asema Prof Holmes, itakuwa vigumu sana.

Je, hii inajibu swali la jinsi gonjwa hilo lilianza?
Huu sio uthibitisho wa uhakika. Hilo ni jambo ambalo hatuwezi kuwa nalo.

Utafutaji wa uthibitisho huo wenyewe umekuwa wa kisiasa sana. Ingawa hii inatoa uzito kwa nadharia kwamba virusi viliibuka kutoka kwa wanyama wa porini na kuenea kwa wanadamu kwenye soko, nadharia nyingine imezingatia uwezekano wa "uvujaji wa kimaabara" wa virusi kutoka Taasisi ya Wuhan ya Virology.

Nadharia hiyo ilipata vichwa vya habari tena hivi majuzi baada ya uingiliaji kati wa FBI, wiki kadhaa baada ya tathmini ya kijasusi kutoka kwa idara ya nishati ya Marekani kuhusu asili ya janga hilo.

Katika mahojiano yake na BBC Science in Action, Prof Holmes aliashiria uchunguzi wa awali wa kesi za mapema zaidi za Covid huko Wuhan. "Mlipuko huo ulianza karibu na soko," alisema. "Na sasa tunaweza kuona kwa nini - wanyama muhimu wanahusika.

"Haikuanza karibu na maabara, ambayo iko umbali wa kilomita 30. Na hakuna kipande kimoja cha data kinachoonyesha kesi za mapema karibu na maabara."

Kuchelewa kwa miaka mingi katika kutoa data hii muhimu kumesababisha kufadhaika na kukasirishwa na Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa cha China (CDC).

"Takwimu hizo ni za miaka mitatu - ni kashfa kabisa kwamba imechukua muda mrefu kuona mwanga," alisema Prof Holmes.

Katika mkutano na waandishi wa habari tarehe 17 Machi, 2023 Tedros Adhanom Ghebreyesus, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni, alisema kwamba "kila data" ni muhimu katika kutusogeza karibu na jibu hilo.

"Na kila data inayohusiana na asili ya Covid-19 inahitaji kushirikishwa kwa jumuiya ya kimataifa mara moja."

"Lazima tuache siasa na kurudi kwenye sayansi safi," Prof Holmes alisema.

Aliongeza: "Binadamu hupata virusi kutoka kwa wanyamapori - imekuwa kweli katika historia yetu yote ya mageuzi. Jambo bora tunaloweza kufanya ni kujitenga na wanyamapori hawa na kuwa na ufuatiliaji bora.

"Kwa sababu hii itatokea tena."
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad