Baba ampachika mimba binti yake na kumuoa, aishi nyumba moja na mama yake
Familia ya Chihinzi Misagwe Ezekiel (baba), Tumaini Chihonzi (binti), na Ntakwinja Kakumba (mama) sio familia ya kawaida kwani mama na binti wameolewa na mume mmoja.
Hali ya kawaida katika familia hiyo iligeuka siku moja Tumaini aliporejea nyumbani akitokea shuleni wakati baba yake alimlazimisha kushiriki mapenzi naye akitishia kukoma kumlipia karo.
"Mama hakuwepo nyumbani; nilienda kuosha na baba akaja chumbani kwangu na kuniambia nilale naye. Nilikataa ombi lake, akaniambia kwa hasira kuwa hatanilipia karo tena," Tumaini aliambia Afrimax English mnamo Februari 18.
"Pia alisema hatawahi kunipa kitu kingine chochote kama mafuta, nguo na kitu kingine chochote ninachohitaji," aliongeza.
Usiwahi kukosa vidokezo muhimu Kwa sababu alipenda shule na alitaka kuendelea na masomo, Tumaini alifanya mapenzi na Ezekiel. Miezi michache baadaye, alimpachika mimba na kumuonya kuwa asimwambie mtu yeyote, hata mama yake.
"Mara ya kwanza nilipogundua kuwa alikuwa mjamzito nilikasirika sana na huzuni wakati huo huo, niliumia sana kwa sababu nilidhani lilikuwa kosa langu.
Nilisisitiza sana lakini hakuniambia na niliamua mara akiwa tayari atanieleza," alisema Kakumba.
Kwa upande mwingine, Tumaini alihuzunika sana na kudhani amemsaliti mama yake. Yeye, baadaye, alimwambia kabla tu ya kujifungua mtoto. “Nilieleza tukio zima na alimkasirikia sana,” alisema Tumaini.
"Mara ya kwanza niliposikia habari hiyo nilikasirika na kuwa na huzuni, nilikasirika sana lakini baadaye niliamua kumtunza binti yangu na mtoto wake," alisema mama huyo aliyefadhaika. Papa Tumaini aomba msamaha
Tumaini na baba yake pia waliomba msamaha na wakasamehewa.
“Mama yangu ni mtu mtulivu sana, alikasirika lakini alimsamehe, nilimuomba anisamehe akafanya hivyo ndiyo maana bado nipo na mtoto wangu. Baba yangu ndiye anatusimamia kifedha,” alisema Tumaini.
Ezekiel anafurahi kwamba familia yake sasa inaishi kwa amani baada ya kilichotokea.
Baba huyo wa watoto 12, bado anataka kuendelea kufanya mapenzi na bintiye lakini Tumiani amekataa. Kakumba sasa anawashauri wasichana wachanga kuepeka hali hiyo kwa kuvaa nguo za heshima wanapotangamana na wengine.