Bamako Wanachakaa Mapema Kwa Yanga Kwenye Uwanja Wa Mkapa, Dar

 


KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ameweka wazi kuwa amepanga kuwatumia washambuliaji wake wawili, Fiston Mayele na Kennedy Musonda kwa lengo la kuhakikisha wanapata ushindi wa mapema katika mchezo wao wa leo Jumatano dhidi ya Real Bamako ya Mali.


Nabi ametoa kauli hiyo kuelekea katika mchezo huo wa Kundi D katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambao utapigwa saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, huku katika mchezo wao uliopita timu hizo zikitoka sare ya bao 1-1.


Akizungumza na Championi Jumatano, Nabi alisema kuwa anachokiangalia katika mchezo huo ni namna gani washambuliaji hao wanaweza kumfaidisha kupata ushindi wa mapema katika mchezo huo huku akisisitiza hawezi kuwadharau wapinzani wao kwa kuwa bado wanafasi ya kufanya vizuri.

“Tunachokiangalia kitu cha kwanza ni namna ambavyo tunaweza kupata matokeo katika mchezo wa Jumatano (leo) kwa sababu tutakuwa tunacheza nyumbani lakini ndiyo mchezo ambao tunaamini unaweza kutupa njia ya wapi tunakwenda hivyo lazima tuhakikishe matokeo mazuri yanapatikana.


“Nadhani sasa ni wakati wa safu ya ushambuliaji kutimiza majukumu yake hasa kwa yale ambayo tumekubaliana katika uwanja wa mazoezi, yupo Mayele, Musonda na hata kwa Mzize (Clement) kwa sababu tunahitaji ushindi wa mabao ya mapema ili kuweza kumaliza mchezo tukiwa katika wakati mzuri zaidi,” alisema Nabi ambaye alisema kwenye mchezo huo atawakosa nyota Sure Boy ambaye ana msiba wa mtoto wake na Jesus Moloko ambaye aliumia kwenye mchezo dhidi ya Prisons akitarajiwa kuangalia kwenye mazoezi ya jana jioni kama atakuwa fiti kucheza.


NJIA YA ROBO FAINALI


Wakati Nabi akizungumza hayo, naye Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe ameliambia Championi Jumatano kuwa: “Ikiwa tulishinda mchezo wa kwanza nyumbani (vs TP Mazembe, 3-1) na kuongeza nguvu ya kujiamini kwenye mchezo wetu dhidi ya Real Bamako huu ni muhimu kwetu utafungua njia ya kufika hatua ya robo fainali.


“Kwa upande wa wachezaji, benchi la ufundi hapa kila mmoja anatimiza majukumu yake kwa umakini Imani yetu ni kuona tunapata ushindi kwenye mchezo wetu mgumu.”

AZIZI KI SHANGWE TUPU

Kiungo aliyeipeleka Yanga hadi makundi, Aziz Ki alisema: “Wachezaji pamoja na benchi la ufundi wote kwa pamoja tupo fiti na tayari kuipambania timu na kupata pointi tatu muhimu.

“Tunaamini ni mchezo mgumu kwa pande zote kutokana na kila moja kujiandaa, lakini kwetu itakuwa nafuu kutokana na sapoti kubwa tutakayoipata kwa mashabiki wetu.

“Niwatake Wananchi wajitokeze kwa wingi hiyo kesho (leo) kwa ajili ya kutusapoti, kwani shabiki ni mchezaji wa 12 tutakapokuwepo uwanjani,” alisema Aziz Ki.

KUNDI LA YANGA CAF

P    W D   L    GF GA Pts


US Monastir   3    2    1    0    5    1    7

2.Yanga               3    1    1    1    4    4    4


3.TP Mazembe           3    1    0    2    4    6    3


4.Real Bamako            3    0    2    1    3    5    2


RATIBA YAO


Leo Jumatano


Yanga v Real Bamako 1:00 Usiku


Machi 19, 2022


Yanga v Monastir 1:00 Usiku


Aprili 2, 2022


TP Mazembe v Yanga

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad